Muungano wa walimu wa shule za kibinafsi kaunti ya Taita Taveta
Sasa umetoa wito kwa serikali ya kitaifa na wazazi walio na wanafaunzi katika shule hizo kuwasaidia wakati huu mgumu wa janga la covid-19.

Naibu mwenyekiti wa muungano huo Francklin Kavi amesema kuwa kwa sasa bado walimu hao hawajapata usaidizi wowote hata baada ya kutembelea ofisi husika katika kaunti hii.

Kulingana na baadhi ya walimu hao wanaofundisha shule za kibinafsi kaunti hiyo wanasema kwa sasa wengi wao wameshindwa kulipa kodi za nyumba na sawia na bima ya kitaifa ya Matibabu.

Masaibu ya Walimu hao wa shule za kibinafsi yalijiri  baada ya shule zote kufungwa nchini kama hatua ya dharura ya kuzuia msambao wa virusi vya ugonjwa wa corona.

Picha kwa hisani

By By Mwadime Iryne

Multimedia journalist

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *