HARARE

Soko la hisa nchini Zimbabwe limerejelea shughuli zake za kawaida baada ya mwezi mmoja likiwa limefungwa ili kusaidia sarafu ya nchi hiyo kupanda wakati ambapo Zimbabwe inakumbwa na kipindi kigumu kiuchumi.

Kwa zaidi ya mwongo mmoja Zimbabwe imekuwa na hali ngumu ya kiuchumi na kushuhudia idadi kubwa raia wake kukosa kazi.

Wakati huo huo wauguzi mjini Harare na katika baadhi ya miji wameendelea na maandamano yao kulalamikia mazingiria mabovu ya kufanya kazi na mishahara duni raia nao wakiandamana kuishinikiza serikali kuu kuboresha maisha yao kwa kuinua uchumi.

JUBA

Shirika la kuwahudumia watoto duniani UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya taifa changa sana Duniani Sudan kusini limeanzisha zoezi la kuwaelimisha kina mama Sudan kusini kuhusu umuhimu wa kuwanyonyesha watoto.

UNICEF inasema kwamba watoto milioni tano nchini Sudan Kusini wanakosa lishe bora.

Maafisa wa afya wa Sudan Kusini wanasema kuwa kina mama wengi hasa wale wanaojifungua wakiwa katika hospitali za kibinafsi hushauriwa kuwapa watoto wao maziwa ya unga yanayonunuliwa dukani badala ya maziwa ya mama, hii ikiwa njama ya wauguzi na watengeneza maziwa hayo kupata soko la bidhaa zao.

Maziwa ya mama hasa katika miezi sita ya kwanza humsaidia mtoto kuimarisha kinga ya mwilini pamoja na kuwaongozea virutubishi muhimu

N’Djamena

Wizara ya habari na mawasiliano nchini Chad imepunguza kasi ya mtandao kote nchi ili kupunguza uvumi, habari za uongo na jumbe zenye kuleta mgawanyiko ambazo zimeibua vita vya uhasama wa kikabila.

Msemaji wa serikali Mahamat Zene amesema hatua hiyo mpya kupunguza kasi ya huduma za internet italegezwa hivi karibuni joto la kikabila litakapopungua.

Kulingana na mhudumu mmoja wa shirika la mawasiliano ambaye hakutaka kutajwa, serikali ilifikia hatua hiyo baada ya kanda ya video kusambaa mtandaoni.
kanda hiyo iliimwonyesha afisa wa jeshi kutoka kabila lenye watu wengi nchini humo akiwafyatulia risasi mafundi wa kutengeneza magari baada ya kuzozana na hatimaye raia kumvamia afisa huyo kwa kumdunga kisu japo alinusurika kifo huku fundi mmoja akipoteza maisha yake.
…………………..

By By Henix Obuchunju

Multimedia journalist

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *