Kizazaa kilizuka katika boma moja huko  ikolomani kaunti ya kakamega,baada ya wake wenza kuzozania maiti ya mume wao.

Mke wa kwanza ambaye huishi Nairobi alifika bomani humo akiandamana na wanawe watano na kuanza kuomboleza mumewe lakini mke mwenza alidinda kumruhusu kuingia katika boma hilo.

Boma hilo liko chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi huku mke wa kwanza akisema kuwa mila na desturi za waluyia zinamruhusu kumiliki kikamilifu mwili wa mumewe.

Jamaa za marehemu hata hivyo wanadai  mke huyo wa kwanza alikuwa ameachana na mumewe kabla ya mauti kumpata.

By Mwadime Iryne

Multimedia journalist

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *