47 Swahili
Aliyekuwa Mhandisi Katika kampuni ya Google Ahukumiwa

Aliyekuwa mhandisi katika kampuni ya Google Antony Levandowski amehukumiwa kifungo cha miezi 18 kwa kuiba siri za kibiashara.
Levandowski anatuhumiwa kwa kuiba siri za kibiashara na kufanya kazi kutoka kwa kampuni ya Google Alphabet iliyokuwa inaongoza huduma za magari ya kujiendesha ya Waymo na kupeleka siri hizo kwenye kampuni pinzani ya Uber alipojiunga nayo.
Kwenye kikao cha mahakama, Levandowski alikubali kulipa dolar 756, 499 kama fidia kwa Waymo pamoja na faini ya dola 95,00.
Multimedia journalist
47 Swahili
Mazishi Bila Maiti

Familia moja katika kijiji cha Onyakoboke, Wadi ya Riana katika kaunti ya Kisii inahuzunika baada ya kupokea Habari iliyodai mwana wao ameaga dunia kule Al Hofuf, Saudi Arabia mwezi jana.
Kulingana na familia hiyo ya Mary Bonareri na Christopher Nyanchabera, walipokea simu mnamo Octoba 9 2020 ikiwajulisha binti yao, Janet Nyanchabera, amefariki kutokana na Covid-19 kwenye nchi hiyo ya Kiarabu ambako alikuwa ameajiriwa kama dereva.
Hata hivyo, siku 30 baadaye, familia ya Mary haijaamini ujumbe huo kwani hawajapokea maelezo kamili kutokana na madai ya kifo cha mwanao.
“Janet alielekea Saudi kutafuta kazi ili asaidie familia yetu ambayo ni maskini. Mwezi moja umepita tangu tupokee simu kwamba amekufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19. Tumekesha hapa nyumbani tukiomba na kutumaini kuwa msamaria mwema atajitokeza na kutuletea mwili wa mtoto wangu nyumbani. Lakini tunaendelea kupoteza matumaini kwa vile ni vigumu kuomboleza bila maiti. Hata tumeanza kufikiria kubomoa vibanda kwenye boma ndiposa tukae tukijua hatuna matanga,” alisema Bi Bonareri kwa uchungu mwingi
Mary Bonareri akiwa nyumbani kwake. Picha: Cindy Odinga
“Aliposafiri, hatukupata kuelewa ajenti yake alikuwa nani kwa vile aliondoka kisirisiri. Ninaomba serikali ya Kenya itusaidie,” Bi Bonareri liongeza.
Walipotembelewa na 47 reporters, Christopher Nyanchabera ambaye ni babake Janet, alikuwa na mshtuko mkubwa hivyo hangeweza kuzungumza .
Kulingana na Denise Nyanchabera, kakake mdogo Janet, yeye ndiye alikuwa wa mwisho kuwasiliana na dadake Septemba 23 2020. Siku hiyo, Janet alimfichulia kuwa alikuwa mgonjwa. Hata hivyo, Denise anasema dadake hakumweleza anaugua ugonjwa upi.
Janet hakuwahi wasiliana tena na mtu yeyote wa familia. Aliyepiga simu, akitumia nambari +966 53 00331777 , alikuwa mwajiri wake “boss” Janet, akieleza kifo cha mwendazake.
Bosi huyo hajakuwa tayari kusimulia ni vipi Janet aliaaga dunia.
Nduguye mkubwa Janet, Jared Oyugi, anakumbuka alikuwa amepinga kusafiri kwa dadake kuelekea Ughaibuni na hata kuficha cheti chake cha kuzaliwa. Hata hivyo, dadake hakusikiliza mawaidha yake. Jared anasema Janet alijitafutia vyeti feki na hata kubadilisha jina lake likawa Janet Wanjiku Nyamburi.
Licha ya hayo, Bw Oyugi anaiomba serikali ya Kenya, ikishirikiana na ile ya Saudi Arabia, ziwasaidie na maelezo tosha kuhusu kifo cha mwanao ili waweze kurejelea maisha yao ya kawaida.
“Ombi letu ni kwamba tumzike hapa nyumbani na tumuage kwa mara ya mwisho; ili tuweze kuridhika kwamba ametuacha. Tulijulishwa kwamba alikufa kutokana na Covid-19 ila ni vigumu kuamini kwa vile hakuna mtu yeyote katika familia yetu ambaye ameona hata picha ya maiti. Hatujaamini kwamba amekufa,” Bwana Oyugi aliambia 47 reporters
Waliokongamana nyumbani kwa Mwendazake wasijue la kufanya. Picha: Cindy Odinga
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya mwendazake Joseph Mukora alisema jamii yao haijawahi kufkiwa na msiba kama huu wa mmoja wao kufariki akiwa nje ya nchi. Anaiomba serikali iingilie kati, iwapo ni kweli Janet ameshafariki.
“Matumaini yetu ni kumzika nyumbani kwa wazazi wake kulingana na mila na desturi za jamii ya Abagusii lakini hatuna uwezo wa kifedha,” Bw Mukora alisema.
Hadi sasa, mipangilio ya mazishi imesimama. Hawajui la kufanya.
Multimedia journalist
47 Swahili
Polisi Wanawasaka Watu Waliowauwa Fisi Huko Narok

Polisi wameanza Mchakato wa kuwasaka majangili wanne waliowauwa fisi watatu,simba wanne na swara katika mbuga ya wanyama ya olchoro olorua narok.
Afisa wa kulinda wanyama pori katika kaunti hiyo ya Narok amesema majangili hao waliweka mitego mingine 25 ambayo iliteguliwa na mafiasa wa polisi.
Msimazi wa KWS katika kaunti hiyo ya Narok richaed chekwani amesema mgogoro unaoshuhudiwa kati ya binadamu na wanyama pori unatokana na binadamu kuweweka maakazi karibu na makaazi ya wanyama pori.
Multimedia journalist
47 Swahili
Maajabu! Wake Wenza Wazozania Mwili wa Mume Aliyeaga

Kizazaa kilizuka katika boma moja huko  ikolomani kaunti ya kakamega,baada ya wake wenza kuzozania maiti ya mume wao.
Mke wa kwanza ambaye huishi Nairobi alifika bomani humo akiandamana na wanawe watano na kuanza kuomboleza mumewe lakini mke mwenza alidinda kumruhusu kuingia katika boma hilo.
Boma hilo liko chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi huku mke wa kwanza akisema kuwa mila na desturi za waluyia zinamruhusu kumiliki kikamilifu mwili wa mumewe.
Jamaa za marehemu hata hivyo wanadai  mke huyo wa kwanza alikuwa ameachana na mumewe kabla ya mauti kumpata.
Multimedia journalist
-
Education4 years ago
Exposed: Inside university of missing marks, chaos and delayed certificates
-
Media2 years ago
Milele FM Reshuffles Presenters
-
Culture4 years ago
Amnesty International Kenya statement on Court of Appeal decision upholding LGBTI Rights organisation’s right to register
-
County News2 years ago
Nyamira KCSE Candidates Under Probe Over Chemistry Exam Leakage
-
47 Swahili3 years ago
Polisi Wanawasaka Watu Waliowauwa Fisi Huko Narok
-
County News4 years ago
Where to live in Kisii town according to the depth of your pocket
-
Counties3 years ago
Nyawawa:The dreaded ghosts that ensured curfew in Kisumu at the weekend
-
47 Swahili3 years ago
Habari Muhimu za Bara Afrika