Iwapo wewe mi mhudumu ama mmiliki wa baa utahitajika kufunga biashara hiyo kuanzia hii leo hadi wakati usiojulikana. Haya ni kwa mujibu wa rais uhuru kenyatta katika hotuba yake hii leo .
Rais kenyatta amesema wenye mikahawa na hoteli hawataruhusiwa kuuza vileo kuanzia usiku wa leo,na kwamba iwapo yeyote atapatikana basi atanyanganywa leseni za kuhudumu na kukabiliana na mkono wa sheria.
Hata hivyo kafyu itaendelea kuzingatiwa hadi siku 30 zijazo pamoja na marufuku ya mikutano yote ya hadhara .
Aidha rais ameshtumu vikali wakenya wanaochukulia janga la covid19 kuwa si hatari na kupuuza maagizo ya wzara ya afya kuzuia msambao wa virusi vya corona.
Vilevile amewaomba wakenya kushikamana na kujali kila mmoja na kutilia maanani masharti hayo yaliyowekwa na wizara ya afya
Picha zote kwa hisani